Siku
moja baada ya bunge nchini Rwanda kupitisha rasmi mependekezo ya
kufanyika marekebisho kwenye katiba ya nchi hiyo ili kumpa nafasi
nyingine rais Paul Kagame kuwania urais kwa muhula wa tatu mfululizo,
serikali ya Marekani imelaani hatua hiyo ya bunge la Seneti.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya kigeni ya
Marekani, haikusema wazi iwapo misaada ya Marekani kwa nchi ya Rwanda
itasitishwa lakini ikaonya kuhusu kupitiwa upya kwa mikataba ya
ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Marekani
inamtaka rais Kagame kuheshimu kile alichowahi kukisema kuhusu
kuendelea kizazi kijacho cha Rwanda kwenye utawala, na kuachana na
mpango wake wa kuwania urais mwaka 2017.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire