Rais
wa Nigeria, Muhammadu Buhari, anasema kuwa jeshi lake lilinyimwa
silaha na misaada mingine ya kijeshi kukabiliana na kundi la Boko
Haram na maelfu ya raia kupoteza maisha kwasababu kulikithiri vitendo
vya rushwa wakati wa ununuzi wa baadhi ya vifaa.
Rais
Buhari amesema kuwa anataka wale wote watakaobainika kuwa walihusika
katika kashfa hiyo ya mamilioni ya fedha wakati wa ununuzi wa zana za
kijeshi, kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, kauli anayoitoa punde
baada ya kupokea ripoti ya tume iliyoundwa kuchunguza tuhuma za
rushwa ndani ya jeshi.
Ripoti
hiyo imeonesha kuwa kulikuwa na mazingira tatanishi ya manunuzi ya
zana hizo kwakuwa amri ya kununua vifaa ilitolewa wakati jeshi likiwa
kwenye mapambano na wapiganaji wa Boko Haram kaskazini mwa nchi hiyo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire