Wanajeshi
wawili wa Tchad waliomo katika kikosi cha umoja wa afrika nchini
Jamhuri ya afrika ya kati Misca, wamepoteza maisha jana Jumapili
jijini Bangui wengine wawili wamejeruhiwa wakati wa makabiliano
baina yao na waasi wa kikristo wa kundi la Anti Balaka.
Duru
za jeshi za Umoja wa Afrika zimearifu kuwa wamajeshi hao walirusihiwa
guruneti na waasi hao wa anti balaka, jana jumapili huku mwanajeshi
mwingine akijeruhiwa katika mapigano mapya ya leo jumatatu.
Kwa
mujibu wa jenerali Martin Tumenta kamanda wa operesheni ya majeshi ya
Misca, wanajeshi hao walikuwa wakitembea kwa mguu katika kata moja
jijini Bangui kabla ya kurushiwa guruneti. Hata hivyo amesema
kiongozi huyo kwamba wanajeshi hao walikuwa hawanaruhusa ya kutembea
katika kata hiyo
Hayo
yanajiri wakati hapo jana viongozi wa kundi la anti Balaka
wanaozuiliwa katika jela kuu jiijini Bnagui walijaribu kutoroka bila
mafaanikio baada ya kupata msaada kutoka kwa kiongozi wa jela hilo.
Kulingana na taarifa iliotolewa na vikosi vya Misca jijini Bangui,
wanajeshi wa Rwanda walikuwa makini na kuvumbua mpango huo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire