Wananchi
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wamegawanyika kuhusu uamuzi
wa rais Josephu Kabila kutangaza msamaha kwa wapiganaji wa kundi la
waasi wa M23 waliofurushwa mashariki mwa nchi hiyo mwezi December
mwaka jana.
Kufuatia
hatua hiyo wapo wananchi wanaounga mkono huku wengine wakionesha
kuchukizwa na kitendo hicho kwa kile wanachodai waasi hao hawakupaswa
kupewa msamaha kutokana na makosa waliyotekeleza.
Mary
Robinson balozi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN kwa
nchi za maziwa makuu, yeye anapongeza uamuzi wa Serikali ya Kinshasa
kuwaachia huru waasi wa M23.
"Nimefurahishwa na Hili,
nadhani ni kwa ajili ya kuhakikisha Amani ya kudumu inapatikana
katika ukanda Huu Mzima. Pamoja na kundi la M23 tulipiga Hatua hadi
kupata mafanikio makubwa ya Amani kuhusu masuala ya kijeshi na pia
kwa kadiri tulivyokuwa wenye kuendelea na mazungumzo ya Kampala.
Nimefurahi sana kuona Bunge la kitaifa limepasisha muswada wa Sheria
ya msamaha, ninajua haikuwa rahisi Bali ni kwa Jina la Amani, ndio
inatubidi kuendelea Mbele."
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire