Pages

mardi 18 février 2014

WAKIMBIZI WA DRCONGO WALIOKUWA WAMEKWAMA HUKO BANGUI WAREJESHWA MAKWAO NA UNHCR


Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi duniani UNHCR limesema kuwa limefanikiwa kuanza zoezi la kuwahamisha wakimbizi kutoka nchini DRCongo waliokuwa wamekwama jijini Bangui Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwapeleka hadi mji wa Zongo Upande wa DRC, karibu na Mpaka baina ya mataifa hayo mawili.

Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Shirika hilo la UNCHR Jijini Kinshasa Céline Schmitt amesema wengi baadhi ya wakimbizi hao raia wa DRCongo walikimbia mapigano katika Mji wa Bangui, wakati kundi la wapiganaji wa Seleka walipofanya mapinduzi ya kijeshi, nao walisafirishwa kwa awamu mbili tofauti Kutoka Bangui hadi mjini Zongo, katika jimbo la Ikweta.

Msemaji huyo ameongeza kuwa awamu itakayofwata itakuwa ni kuwasafirisha wakimbizi hao hadi miji na vijiji vyao vya Libenge Huko DRC.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...