Rais wa mpito nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza, amesema kuridhishwa na hatuwa ya raia wa Ufaransa kupitia wawakilishi wao bungeni na kwenye baraza la seneti kupiga kura ya kuidhinisha kuendelea kuwepo kwa majeshi ya Ufaransa nchini mwaka. Reuben Lukumbuka na maelezo zaidi.
Rais
Catherine Samba Panza amempongeza rais wa Ufransa Francois Hollande
kwa juhusdi anazo zifanya kuhakikisha usalama na utulivu vinarejea
jijini Bangui na vitongoji vyake.
Kufuatia
hatuwa hiyo rais Panza amelihutubia taifa jumatano hii ambapo
amewatolea wito makundi yote ambayo bado yanamiliki silaha
kujisalimisha kabla ya kuchukuliw ahatuwa kali.
Hapo
jana bunge la Ufaransa limeidhinisha kuongezwa muda wa kuwepo kwa
vikosi vya Ufaransa vilivyopo katika operesheni Sangaris nchini
Jamhuri ya Afrika ya kati.
Hivi
karibuni Catherine Panza aliomba muda wa uwepo wa vikosi hivyo nchini
humo uongezwe kufuatia kuendelea kuripotiwa kwa vitendo vya mauaji ya
kidini dhidi ya raia waumini wa kiislam.
Mbali
na kuongezwa muda kwa vikosi hivyo vya Ufaransa, Wito umeendelea
kutolewa nchini humo wa kuongeza idadi ya majeshi hayo pamoja na yale
ya Umoja wa Afrika kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya mauaji ya
kuvizia.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire