Msanii nguli wa Muziki wa Rumba nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo King Kester Emeneya amefariki
mapema leo alhamisi asubihi katika Hospitali Marie Lannelongue
jijini paris nchini Ufaransa.
Jean
Emeneya Mubiala Kwamandu, Maharufu kama King kester Emeneya ambaye
amezaliwa Novemba 23 mwaka 1956 mjini Kikwiti ambapo alisoma kwenye
chuo kikuu cha Lubumbashi katika mwaka 1977 alijiunga na bendi ya
Viva la Musica ambapo aliimba baadhi ya nyimbo zilizo msababishia kupata sifa
tele na hivo kuwa msanii nyota katika mwaka 1980 na baadae akaunda
bendi yake Victoria Eleyson Desemba 24 mwaka 1982.
Kwa
mujibu wa duru za familia ya kiongozi huyo wa bendi ya Victoria
Eleison alikuw amelazwa katika Hospitali moja huko Paris tangu mwezi
Novemba kufuatia matatizo ya moyo . Kester Emeneya alikumbwa na
mshtuko mkubwa wakati alipo pokea kifo cha Tabu ley Rochereau ambaye
alikuwa swaiba wake.
Ma daktari wa Hospitali hiyo walimzuia kuondoka Hospitalini tangu kutoweka kwa Rochereau Novemba 30 mwaka jana na hivo kusalia Hospitanini hadi mapema jana alhamisi asubuhi Februari 13 ndipo amepoteza maisha
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire