Idadi
ya watu waliopoteza maisha katika mafuriko yaliotokea nchini Burundi
huenda ikaongezeka kufuatia baadhi ya watu hadi sasa hawajulikani
walipo.
Duru
za serikali zimearifu kwamba watu zaidi ya 60 wamepoteza maisha
kufuatia mafuriko hayo yaliosababishwa na mvua kubwa zilizo nyesha
katika usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu.
Hapo
jana waziri wa Usalama wa raia Jenerali Gabriel Nizigama alitaja
idadi ya watu 51 ndio walipoteza maisha baada ya kuangukiwa na kuta
za nyumba zao na wengine kupelekwa na maji, eneo lililoa athirika
zaidi ni kaskazini mwa jiji la Bujumbura.
Msemaji
wa shirika la msalaba mwekundu nchini Burundi Alexis Manirakiza
amesema wamehesabu miili ya watu 60 waliopoteza maisha wengi wakiwa
ni watoto bila hata hivyo kutaja idadi ya watoto hao.
Polisi
nchini Burundi imesema Hii ni mara ya kwanza kutokea kwa maafa ya
aina hii kutokana na mafuriko na hofu imetanda huenda idadi ya watu
waliopoteza maisha ikaongezeka, kutokana na taarifa za mafuriko
katika Miko mingine ya taifa hilo. Burundi wakati huu ipo katika
msimu wake wa mvua.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire