Pages

mercredi 19 février 2014

WANAHARAKATI NCHINI AFRIKA KUSINI WAWATEA RAIA WAWILI WA UGANDA WAIRUDISHWE NCHINI KWAO


Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Afrika Kusini yameitaka serikali kutowarudisha nyumbani raia wawili wa Uganda, mmoja akiwa ni daktari na mwingine ni mwanaharakati wa kutetea ndoa za jinsia moja kuhofia usalama wao.

Daktari, Paul Nsubuga Semugoma hapo jana alijikuta akizuiliwa na maofisa wa uhamiaji wa Afrika Kusini baada ya kutolewa ombi na Serikali ya Uganda kutaka arejeshwe nyumbani yeye pamoja na mwanaharakati anayetetea ushiga nchini Uganda.

Semugoma amesema kuwa anahofia usalama wake iwapo atarajeshwa nyumbani kwakuwa amekuwa daktari wa kwanza kuwa mstari wa mbele kupinga sheria iliyopitishwa na bunge inayokataza ndoa za watu wa jinsia moja.

Wanaharakati wa Afrika Kusini wanadai kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kunakofanywa na Serikali dhidi ya raia wanaotetea ushoga ama kukosoa Serikali.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...