Evariste Ngayimpenda na Charles Ntitije |
Wafuasi
watatu wa chama cha upinzani cha Uprona nchini Burundi wametiwa
nguvuni jana jumapili wakati polisi nchini humo ikiendesha operesheni
y kuwasambaratisha wafuasi wa chama hicho waliokuwa wamepnga kufanya
mkutano wa chama.
Watu
watatu wa chama hicho Uprona walioondoka serikalini pamoja na polisi
wawili wamejeruhiwa katika purukushani hizo.
Mzozo
kati ya chama cha rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza CNDD-FDD na
chama Uprona, unatishia hatuwa ya ugavi wa madaraka baina ya watu wa
kabila la wahutu waliowengi na Watutsi waliowachache ambao kumekuwa
na tabu kubwa ya maridhiano baina ya makabila hayo mawili baada ya
kushudia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe miaka kadhaa iliopita.
Wachambuzi
wa siasa wanaokuwa mvutano huo wa chama tawala na chama Uprona
unaweza kurudisha nyuma juhudi zilizopigwa hadi sasa katika kutafuta
maridhiano kama anavyoeleza hapa Omar Khalfan mchambuzi wa siasa za
kimataifa na muhadhiri katika chuo kikuu cha nchini Rwanda.
Polisi
nchini humo iliwasambaratisha wafuasi wa chama Uprona waliokuwa
wamekusanyika katika makao makuu ya chama Uprona ambako ulikuwa
unafanyika mkutano wa kamati kuu.
Baada
ya mvutano, polisi ililazimika kutumia nguvu kwa kuwanyuka viboko
wafuasi hao na kutumia bomu za kutowa machozi ili kuwasambaratisha.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire