Baada
ya mwenyekiti zamani wa chama tawala nchini Burundi Hussein Radjabu
kujitokeza kwenye vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa ikiwa ni
majuma kadhaa baada ya kuwepo kwa taarifa za kutoroka jela na kutowa
wito kwa Jumuiya ya kimataifa kutovumilia uvunjifu wa sheria ya
Burundi kwa kumruhusu Nkurunziza kuwania uchaguzi kwa muhula wa 3,
serikali imesema Hussein Radjabu ni mtu anaependa uasi, hivyo hana
nafasi kwa sasa nchini Burundi.
Hussein
Radjabu Mwenyekiti zamani wa chama tawala nchini Burundi cha
CNDD-FDD amezungumza kwa mara ya kwanza tangu kuwepo na taarifa za
kutoroka kwake katika jela kuu la Mpimba jijini Bujumbura.
Akihojiwa
na idhaa mbalimbali za kimataifa, Hussein Radjabu amesema Kwa sasa
yupo katika eneo salama, pamoja na wananchi.
Katika
mahojiano hayo, Hussein Rajabu amesema hakutoroka jela kama
inavyoelzwa huku na kule bali kilichotokea faili lake lilikuwa
tayari, lakini rais Nkurunziza alikuwa bado amebana kwa sababu
azijuazo mwenyewe, lakini kutokana na watu wa karibu waliokuwa pamoja
katika harakati za kuwania demokrasia, hawakupenda kuona naendelea
kueshi katika jela katika kipindi hiki ambacho kulikuw ana mpango wa
kuendesha vurugu katika jela ili wamzuri.
Akieleza
namna alivyoondoka katika jela kuu ka mpimba, kinara huyo zamani wa
CNDD-FDD amesema aliondoka kwa heshima na tahadhwima hadi eneo alipo
kwa wakati huu.
Akizungumzia
kuhusu hali ya siasa nchini mwake na iwapo ana nia ya kurejea
nyumbani kushiriki kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi
June mwaka huu, mwenyekiti huyo wa zamani wa CNDD-FDD amesema tatizo
lililopo sio ushiriki wake au la bali ni utawala uliopo hautaki
kuheshimu misingi ya demokrasia.

Willy Nyamitwe msemaji wa rais Nkurunziza
Aidha,
kongozi huyo ametowa wito kwa raia na wanasiasa wa Burundi
kushikamana ili kuboresha hali ya kisiasa iliopo nchini Burundi
ambapo amesema hakuna kinachoendeka, kila kitu kipo katika hali ya
sintofaham, hususan maandalizi ya uchaguzi.
Upande
wake serikali ya Burundi imesema Radjabu bado hajamaliza kutumikia
kifungo chake na kwa vile ni mtu hatari ambaye anaweza kutishia amani
nchini Burundi, serikali inajipanga kukabiliana na hali yoyote hiyo
kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika hali tulivu.
Msemaji
wa rais Nkurunziza kupitia radio ya dunia RFI mapema leo asubuhi
amesema Radjabu ni mtu anaefahamika kuwa na tabia ya kuunda makundi
ya uasi, hivyo katika kipindi hiki hana nafasi.

Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire