Kiongozi
wa upinzani nchini Burundi wa chama cha FNL tawi lisilo tambulika na
serikali Agathon Rwasa ametowa wito kwa tume ya uchaguzi nchini humo
kuongeza muda wa zaidi kwa wagombea kuwasilisha faili zao, wakati
huu tume ya uchaguzi CENI ikianza kupokea faili za wagombea katika
chaguzi mbalimbali.
Agathon
Rwasa amesema kutokana na muda wa majuma mawili na idadi ya wagombea,
muda uliotolewa hautotosha, hivyo unahitajika muda zaidi. Rwasa
ametuhumu pia baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakiwazuia kuwafikia
wafuasi wao na hata kuwahutubia.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire