Kiongozi
wa zamani wa chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD Jeremie
Ngendakumana amesema mwenyekiti wa sasa wa chama hicho Pascal
Nyabenda anavunja sheria za chama katika kuwafuata uanachama wafuasi
wa chama hicho wanaopinga hatuwa ya muhula wa 3 kwa rais Pierre
Nkurunziza.
Jeremie
Ngendakumana amemshauri kiongozi huyo wa chama tawala kuwaleta pamoja
wafuasi wote wa chama hicho na kujadiliana kwa pamoja kuhusu muhula
huo wa 3 wa rais Nkurunziza unaoleta utata.
Kuhusiana
na swala hilo la Muhula wa 3, Jeremie Ngendakumana amesema mkataba wa
Arusha upo wazi, hakuna rais anaeruhusiwa kuwania mihula 3.
hayo
yanajiri wakati huu aliekuwa msemaji wa chama cha CNDD-FDD Onesime Nduwimana akiondolewa kwenye uadhifa wake kama mkurugenzi mtendaji
na msimamizi wa shirika la bima SOCABU.
Katika
hatuwa nyingine Ofisi ya haki za Binadamu nchini Burundi imefahamisha
kwamba inafuatilia kwa karibu zaidi taafiza za uwepo wa vitishi na
vitimbi dhidi ya wale wote waliobaini msimao wao wa ku0inga muhula wa
3 kwa rais Pierre Nkurunziza
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire