Pages

vendredi 17 avril 2015

POLISI YATUMIA NGUVU KUZIMA MAANDAMANO JIJINI BUJUMBURA WATU 3 WAKIWEMO POLISI WAJERUHIWA

Askari polisi wawili wamejeruhiwa huku watu zaidi ya kumi wakitiwa mbaroni jijini Bujumbura hii leo Ijumaa wakati polisi ilipokuwa ikijaribu kuzima maandamano ya upinzani unaopinga hatuwa ya rais Pierre Nkurunziza kutaka kuwania muhula wa 3 wa rais, jambo ambalo linaelezwa kuwa kinyume cha sheria mama ya nchi hiyo.

Licha ya kwamba rais Nkurunziza hajajitangza rasmi kuwania muhula huo wa 3, upoinzani na mashirika ya kiraia yanamtuhumu kuonyesha dalili za kuwania nafasi hiyo licha ya kushauriwa na wanadiplomasia kutoka ndani na nje ya Burundi.

Mwenyekiti wa heshima wa chama cha upinzani cha UPD Zigamibanga Chavino murwengezo ambae alijiunga na waandamanaji jijini Bujumbura amesema, polisi imewazuia kuandamana kwa amani, wakati juma lililopita polisi hiyo iliwaliandia Usalama wale wanaounga mkono muhula wa 3.

kiongozi huyo wa Heshma wa UPD ambae aliandamana pamoja na viongozi wengine wa upinzani amesema maandamano hayo yataendelea hadi pale rais Nkurunziza atapo salim amri.

Polisi imetumia maji na mabomu ya kutoa machozi katika kuwatawanya waandamanaji huku mwanamke mmoja akiripotiwa kupoteza fahamu kutokana na moshi wa bomu hizo za kutowa machozi.


Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...