Pages

vendredi 17 avril 2015

UMOJA WA MATAIFA WASEMA WARUNDI ZAIDI YA ELF 8 WAKIMBILIA NCHINI RWANDA NA DRCONGO

Umoja wa Mataifa umesema kwamba zaidi ya watu 8000 wameitoroka Burundi katika kipindi cha majuma mawili yaliopita kutokana hofu ya kutokea mchafuko wakati huu nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais.

Msemaji wa shirika la Umoja wa mataifa linalo hudumia wakimbizi duniani UHCR Adrian Edwards amesema katika mkutano na waandhisi wa habari kwamba jumla ya warundi zaidi ya elf 7.099 wamevuka mpaka kuingia nchini Rwanda huku 1.060 wakikimbilia nchini DRCongo.


ASilimia 60 ya wanaokimbilia nchini Rwanda ni watoto ambao wanawasili wakiwa hawana lolote.


Hofu hii ya wananchi kukimbilia nchini Rwanda imesababishwa na mvutano uliopo wa kisiasa huku vijana wa chama tawala cha CNDD-FDD wa Imbonerakure, wakielezwa kuwa tishio wakati huu mashirika ya kiraia yakitangaza kusubiri tamko la rais Nkurunziza kuwania muhula wa 3 ili waingia barabarani kuopinga kwa nguvu zote hatuwa hiyo.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...