Pages

vendredi 17 avril 2015

UMOJA WA MATAIFA WALAANI MAUAJI YA WAGENI NCHINI AFRIKA KUSINI


Umoja wa Mataifa umesema umeguswa na unalaani mauaji ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini kutokana na mashambulizi yanayoendeshwa na raia wa Afrika Kusini.

Umoja huo wa mataifa umesema kuwa mpaka sasa zaidi ya raia wa kigeni elfu tano wamekimbia makazi yao na machafuko hayo yamesababisha vifo ya watu sita katika miji ya Durban na Johannesburg.


Shirika la umoja wa mataifa la kushughulikia wakimbizi UNHCR limesema kuwa watu walioathirika na machafuko hayo ya kibaguzi ni raia wa kigeni wakiwemo wakimbizi waliokwenda kutafuta hifadhi nchini Afrika Kusini.


Umoja huo umetaka kukomeshwa mara moja mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni kwa sababu wengine walikwenda nchini humo kwa ajili ya kujilinda na kutafuta mahali salama pa kuishi.


Abdulkarim Atiki ni mchambuzi wa siasa za kimataifa na hapa anaangazia hali ya mambo nchini Afrika Kusini wakati huu hofu ikitanda miongoni mwa raia wa kigeni.



Rais wa AFRIKA kusini hiyo jana aliaani mashambulizi na mauaji hayo lakini amekuwa akikosolewa na wanasiasa kwa kutolipa kipaumbele suala hilo.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...