Serikali
ya Afrika Kusini imeahidi hapo jana kuwahukumu wahusika wa machafuko
dhidi ya raia wa Kigeni nchini humo yaliosababisha vifo vya watu
takriban saba tangu mwanzoni mwa mwezi April wakati huu Malawi na
Zimbabwe zikijiandaa kuwarejesha nyumbani raia wake.
Waziri wa mambo ya ndani nchini Afrika Kusini Malusi
Gigaba amesema jana katika mkutano na waandhishi wa habari kwamba
wametuma ujumbe mzito kwa wale waliohusika na machafuko hayo kwamba
watakamatwa na watakiona cha moto.
Kulingana
na waziri huyo watu 307 wametiwa nguvuni tangu mwanzoni mwa machafuko
hayo yalioanza mwishoni mwa mwezi March na ambayo yanawalenga raia wa
Kigeni walioomba hifadhi nchini Afrika Kusini.
Licha
ya kupungua kwa ghasia hizo, katika usiku wa Jumamosi kuamkia
Jumapili kumeshuhudiwa mashambulizi mengine dhidi ya raia wa kigeni
katika miji ya Johanesbourg na D
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire