Pages

mardi 21 avril 2015

MAREKANI YALAANI MASHAMBULIZI DHIDI YA WAGENI NCHINI AFRIKA KUSINI


Mfalme Goodwill Zwelithini wa jamii ya waZulu nchini Afrika kusini aliyetuhumiwa kuwa chanzo cha vurugu dhidi ya wageni amekanusha kuhusika kwake na matukio hayo.

Katika mkutano wa hadhara Zwelithini amekanusha kuhusika katika vurugu hizo na kudai kuwa ametafsiriwa vibaya baada ya kauli yake ya kuomba wageni kufungasha virago na kuondoka nchini humo.

Mkutano wa dharura wa viongozi wa kijadi nchini humo akiwepo mfalme huyo pamoja na mkutano baina yake na mawaziri wa Mambo ya Ndani na wa Usalama yaonekana kuwa chachu ya kukomesha mashambulizi hayo ambapo Mfalme Zwelithini amesema kuwa mashambulizi dhidi ya wageni ni aibu kubwa kwa taifa.

Serikali ya Marekani imelaani jana machafuko ya ubaguzi dhidi ya wageni yanayoshuhudiwa nchini Afrika Kusini na kuwatolea wito viongozi wa nchi hiyo kuchukuwa hatuwa madhubuti kukomesha mashambulizi dhidi ya wageni.

Machafuko hayo yaliwalenga raia wa kigeni waishio nchini Afrika Kusini na kusababisha vifo vya watu 7 na maelfu wengine kukimbia katika miji ya Durban na Johanesbourg.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Marie Harf amesema Marekani kama vile mataifa mengine pamoja na mashirika ua kiraia wanalaani vikali mauaji dhidi ya wageni yanayo shuhudia nchini Afrika Kusini.


Hayo yanajiri wakati huu mataifa kadhaa barani Afrika yakiendelea kujiandaa kuwarejesha nyumbani raia wake waishio nchini Afrika Kusini. Miongoni mwa mataifa hayo ni pamoja na, Malawi, Msumbiji, Zambia, Zimbabwe na Tanzania.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...