Waandamanaji
wamerejea barabarani katika baadhi ya mitaa za manispaa ya jiji la
Bujumbura mapema leo asubuhi baada ya Makataa ya saa 48 yaliyotolewa
na waandamanaji nchini Burundi kumpa nafasi Rais Nkurunziza kufikiria
upya uamuzi wake wa kugombea muhula wa tatu kinyume na katiba na
azimio la Arusha kufikia mwisho.
Taarifa
kutoka Bujumbura zaeleza kuwa waandamanaji katika mitaa ya Buterere,
Musaga, Nyakabiga, Bwiza wamechoma ma tyri barabarani huku katika
tarafa ya buterere risase zikisikika kwa wingi, na huko Kinama
vipeperushi vimesambazwa vinavyo wartia hofu waandamanaji kwamba
ataeandamana basi watakiona cha moto
Tangu
kuanza kwa maandamano hayo April 26 mwaka huu, watu 10 wameuawa
wakati wa maandamano na ambapo shughuli za mazishi kwa baadhi ya
wahanga hao zikifanyika hapo jana ambapo rais wa zamani wa Burundi
Domitien Ndayizeye alisisitiza kuheshimiwa kwa katiba ya nchi.
Wakati
hayo yakijiri, Mkuu wa jeshi nchini humo, Jenerali Prime Niyongabo
akisoma tangazo maalum la jeshi, amerejelea kauli ya waziri wa Ulinzi
Nchini Humo Brigadia Jenerali Pontien Gaciyubwenge siku ya jumamosi,
ambapo amelisifu jeshi nchini humo kwa weledi wake katika kipindi
chote cha maandamano hayo na kulionya kutokuwa na upande wowote.
Wataalamu
wanaona kwamba taarifa ya jeshi ya kutaka viongozi kuheshimu katiba
na mkataba wa Arusha ni ujumbe wa moja kwa moja kwa rais Nkurunziza
ambae kulingana na Upinzani na wanaharakati wa mashirika ya kirai,
anataka kuvunja makubaliano ya Arusha.
Kumekuwa
na mitazamo tofauti kuhusiana na hali inayoendelea nchini Burundi
wakati huu polisi ikiendelea kuwatisha raia kutoandamana, jambo
ambalo linalowafanya raia kuwoana polisi kama adui.
Jumuiya
ya Kimataifa imeonya Burundi
kuhusu
hali inayoendelea kushuhudiwa nchini humo
na kwamba iwapo hatua hazitachukuliwa mapema huenda taifa hilo
likaingi kwenye machafuko.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire