Pages

lundi 4 mai 2015

WATU WAWILI WAUAWA KATIKA MASHINDANO YA KUCHORA VIBONZO VYA MTUME MUHAMAD JIJINI TEXAS


Watu wawili wanaodaiwa kuwa huenda walikuwa wamebeba mabomu wameuawa kwa kupigwa risasi, na polisi mmoja kujeruhiwa nje ya ukumbi ambao kulikuwa kunafanyika mashindano ya kuchora kikaragosi cha Mtume Muhammed mjini Texas, Marekani.

Kwa mujibu wa waandaaji wa mashindano hayo kutoka taasisi ya Marekani ya kulinda uhuru wa kutoa maoni, wamesema kuwa watu hao waliuawa baada ya kurusha risasi kuelekea sehemu ambayo shindano hilo lilikuwa linafanyika na ndipo polisi walipolazimika kutumia nguvu kuwakabili.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hili, wanasema kuwa wakati shindano hilo likiendelea, watu wawili waliokuwa na silaha na vifaa vinavyodaiwa kuwa ni mabomu walianza kusogea kwenye eneo la tukio na kabla ya kufika waliwafyatulia risasi polisi walipkuwa jirani na kuwalenga baadhi ya watu waliohudhuria kabla ya kuuawa na kikosi maalumu cha Polisi wanajeshi.

Polisi mjini Texas wanasema wanaendelea kufanya uchunguzi kubaini sababu iliyowafanya watuhumiwa hao kuwafyatulia risasi waandaaji wa shindano hilo, ingawa baadhi ya watu wamewakosoa watu walioandaa shindano hilo wakijua fika kuwa lazima lingewakera baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu.

Waumini wa dini ya kiislamu wamelaani shambulio hili lakini wakawakosoa waandaaji wa shindano hilo ambalo mshindi alizawadia dola za Marekani elfu 10 kwa kuchora kibonzo wa kinachomuonesha Mtume Muhammad.

Tukio hili linajiri ikiwa ni miezo michache tu imepita toka kushambuliwa kwa ofisi za gazeti la Charlie Hebdo nchini Ufaransa ambalo lilichapisha kibonzo cha mtume Muhammed, ambapo watu wenye silha waliwashambulia wafanyakazi wake na kuua watu 16.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...