Idadi
ya vifo inayotokana na maradhi ya virusi vya Ebola inaelezwa kufikia
zaidi ya watu elfu 1 wakati huu kukiwa na hofu kuwa huenda nchi ya
Nigeria ikawa ni taifa jingine ambalo linakabiliwa na hatari ya
kukumbwa na janga hili wakati huu mgonjwa wa pili akiripotiwa kufa
nchini humo.
Kusambaa
kwa virusi vya ebola kwenye mataifa ya Afrika na baadhi ya mataifa ya
magharibi kunakuja wakati huu ambapo shirika la afya duniani
linakutana na wataalamu wa afya duniani kuamua iwapo watangaze kuwa
ugonjwa wa Ebola ni janga la dunia.
Zaidi
ya watu elfu 1 na 700 kwenye nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone
wamegunduliwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola wakati huu nchi za
Marekani na Saudi Arabia nazo zikiripoti kuwa na wagonjwa wapya.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire