Serikali
ya Jamhuri ya kidemirsia ya Congo imetishia kusitisha shughuli za
kuwarejesha nyumbani wakimbizi takriban elfu 29 wa Angola iwapo
kutaibuka tena dosari mpakani wakati huu viongozi wa Angola wakizuia
watu 66 kuingia nchini kwao.
Mengi
zaidi na Reuben lukumbuka.
waziri
wa mambo ya ndani nchini jamuri ya kidemokrasia ya Congo Richard
Muyej amesema iwapo dosari zitajitokeza tena kama ilivyo shuhdiwa
hapo awali, watasitisha mara moja shughuli hizo na kuomba kukutana na
viongozi wa Angola kwa ajili ya kupanga mikakati mipya kwa ajili ya
kukamilisha shughuli hiyo.
Waziri
huyo amesema anaamini kwamba dosari zipo up-iande wa vingozi wa
Angola.
Takriban
raia elfu 29 wa Angola waliopewa hifadhi nchini DRCongo wamemauwa
kurejea nchini kwa kwa hiari. Wengine elfu 76 tayari wamerejea nchini
kwao tangu mwaka uliopita wakati ilipoanza operesheni ya kuwarejesha
nyumbani zilizoandaliwa na viongozi wa DRCongo, Angola, na Ofisi ya
Umoja wa Mataifa inayowahudumia wakimbizi duniani UNHCR.
Jumanne
juma hili kundi la kwanza lienye wakimbizi 500 liliondoka jijini
Kinshasa kuelekea nchini Angola, lakini walipofika mpakani 182
walizuiliwa mpakani na hivyo serikali ya Congo inaluamu kutokana na
kile ilichokiita udhaifu upande wa Angola katika kukamilisha shughuli
hiyo kwa kutowatuma wataalamu nchini DRCongo kwa ajiloi ya kuwakaguwa
wakimbizi hao, shughuli ilioendeshwa pekee na serikali ya Congo kwa
ushirikiano na UNHCR
Baada
ya mabishano ya muda mrefu, wakimbizi 116 waliruhusiwa kuvuka mpaka,
lakini wengine 66 wakazuiliwa mpakani baada ya viongozi wa mpakani
kukataa vibali walivyopewa kutoka ubalozi wa Angola jijini Kinshasa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire