Siku
moja baada ya kuhitimishwa kwa mkutano wa kimataifa kati ya Marekani
na viongozi wa Afrika ambapo suala la usalama kwenye bara hilo
lilijadiliwa kwa kina na viongozi hao, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
ameendelea kusisitiza nchi yake kutoondoa majeshi yake Somalia.
Rais
Kenyatta amesema kuwa kamwe serikali yake haitavirudisha nyumbani
vikosi vyake vilivyoko Somalia mpaka pale nchi yake itakapo hakikisha
kuwa Somalia ina Serikali yenye nguvu na inayoweza kusimamia mipaka
yake.
Kauli
hii ameitoa wakati akijibu maswali ya raia wa nchi hiyo wanaoishi
Marekani ambapo walitaka kufahamu ni hatua gani Serikali ya Kenya
inachukua kunusuru mashambulizi ya Al-Shabab ambao wanataka wanajeshi
wao kuondoka Somalia.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire