Licha
ya vitisho vya Umoja wa Mataifa vya kutiliwa vikwazo kwa viongozi wa
Sudani Kusini, Pande mbili zinazo zozana nchini Sudani Kusini
zimeshindwa kuunda serikali ya Umoja wa kitaifa kama ilivyoagizwa
katika mazungumzo yaliowakutanisha rais wa Sudani Kusini Salva Kiir
na mpinzani wake Riek Machar na ambapo muda wa mwisho ulikuwa jana.
Mei
9 mwaka huu, Salva Kiir na mpizani wake ambaye aliwa makam wake wa
rais Riek Machar walifikia makubaliano chini ya shinikizo la Jumuiya
Kimataifa kugawana madaraka yalioagiza kuunda serikali ya muungano wa
kitaifa kwa kipindi cha siku 60.
machafuko
na mauaji yenye misingi ya kikabila yameendelea kushuhudiwa nchini
humo tangu desemba mwaka 2013 huku takwimu zikionyesha kuwa watu
zaidi ya milioni moja na nusu wameyatoroka ma kwao kutokana na
machafuko hayo.
Wananchi
wa Sudani Kusini walikuwa na matumaini baada ya kufikiwa kwa
makubaliano hayo, lakini matumaini yameanza kufifia baada ya pande
mbili kushindwa kuweka kando tofauti zao na kutekeleza makubaliano
yao.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire