Wakati wananchi wa jamhuri ya
Afrika ya kati wakisubiri kutangazwa kwa baraza jipya la mawaziri,
wachambuzi wa mambo wanaonakuwa baraza hilo jipya litakabiliwa na
chamgamoto kubwa hususan kupatikana kwa misaada ya kibinadamu na
kuwaunganisha wananchi wa taifa hilo waliogawanyika kwa misingi ya
kikabila na kidini.
Idadi
ya watu waliotoroka makwao kutokana na machafuko yalioikumba nchi
hiyo imeonekana kupungua kidogo ukilinganisha na mwezi Januari mwaka
huu ambapo idadi hiyo ilifikia zaidi ya watu milioni moja. Wakimbizi
waliokimbia katika maeneo ya misitu wakati huu wanakabiliwa na
matatizo chungu nzima hususan ukosefu wa misaada ya kibinadamu huku
wengine wakieshi katika mazingira yenye usalama mdogo.
Mbali
na wakimbizi hao wa ndani kuna idadi nyingine ya raia wa jamhuri ya
Afrika ya kati waliokimbilia nje ya taifa hilo hususan nchini Tchad
na Camaroun ambapo mashirika ya kimisaada yanakadiria kufikia
wakimbizi laki nne ambao wapo nje ya nchi na ambao wengi wao ni
waislam waliokimbia machafuko ya wanamgambo wa Anti Balaka.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire