Pages

lundi 11 août 2014

WAZIRI MKUU WA IRAQ ATANGAZA KUMFUNGULIA MASHTAKA RAIS WA NCHI HIYO


Wakati hali ikiendelea kuwa mbaya kwenye uwanja wa mapambano nchini Iraq kufuatia kundi la Isil kuendelea kujizatiti katika miji kadhaa kaskazini mwa nchi hiyo, mvutano wa wazi umeibuka kati ya rais Fouad Masoum na waziri mkuu Nuri al Malik ambaye ametangaza jana kuwa atamfunuglia mashtaka rais,

Muda mfupi baada ya waziri mkuu wa Iraq Nuri al Malik kutangaza hatuwa yake ya kumfungulia mashtaka rais wa nchi hiyo Fouad Masoum, kwa tuhuma za kukiuka katika ya nchi hiyo, askari wengi wameshuhudiwa katika maeneo muhimu ya jiji la Bagdad.

Duru kutoka jijini Bagdad zimearifu kuwa kwa hali isiokuwa ya kawaida, askari wengi wameonekana katika maeneo ya taasisi za serikali huku barabara kadha za jiji zikifungwa, saa chache baada ya waziri Malik kutangaza ghafla kuwa anaenda kufunguwa mashartaka dhidi ya rais.

Serikali ya Marekani kupitia ujumbe wa Twitter, naibu waziri wa mambo ya nje anayehusika na maswala ya Iraq Brett McGurk, imesema itaendelea kumuunga mkono rais wa nchi hiyo Fouad Masoum ambaye ndiye mlinzi halali wa taasisi za serikali pamoja na waziri mkuu ataye kubalika na pande zote.

Nuri al Malik kutoka jamii ya ma shia ambaye alishinda uchaguzi mwezi April 30 iliopita na ambaye analenga kuwania muhula mwingine wa tatu, amekuwa akikosolewa sana na sera yake ambayo wengi wanasema ni ya kibaguzi dhidi ya watu wa chache wa jamii ya wa Sunni.

Bunge la taifa nchini humo ambalo lilitakiwa kukutana jana kujadili kuhusu swala la kupatikana kwa waziri mkuu anaye kubalika na pande zote, imeahirisha kikao chake hadi Agosti 19 baada ya kutotimia kwa idadi.






Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...