Kituo
cha televishieni cha kundi la Hamas katika ukanda wa gaza
kimefahamisha kwamba Watu 18 wamenyongwa katika ukanda wa Gaza baada
ya kutuhumiwa kushirikiana na Israel. Miongoni mwao, sita wamenyongwa
hadharani, baada ya salama ya Jumaa, tukio lilotekelezwa na watu
walivalia sare ya wapiganaji wa Brigade Ezzedine al Qassam tawi la
kijeshi la kundi la Hamas.
Watu
hao wanatuhumiwa kutowa taarifa kwa jeshi la Israel kuhusu wapi
walipokuwa viongozi watatu wakijeshi wa kundi la Ezzedine al Kassam
waliouawa katika shambulio, huku kiongozi mkuu wa kundi hilo
akinusurika kifo katika shambulio lililogharimu maisha ya watu 3 wa
familia yake.
Hayo
yanajiri wakati huu kiongozi muu wa jumuiya ya waislam Amir wa nchini
Qatar akikutana kwa mara ya pili katika kipindi cha saa 24 na
kiongozi wa mamlaka ya wa Palestina na kiongozi wa Hamas Khaled
Mechaal wakati huu mashmbulizi ya Israel yakiendelea kushuhudiwa
katika ukanda wa Gaza.
Takriban
watu 4 wamepoteza maisha ijumaa hii kufuatia mashambuliz ya vikosi
vya Israel katika ukanda wa Gaza, ikiwa ni siku ya 46 ya mashambulizi
kati ya kundi la Hamas na vikosi vya Hamas.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire