Shirika
lisilokuwa la kiserikali la Voix de sans Voix nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, limsema Watu 11 akiwemo mtetezi wa haki za
binadamu wametekwa nyara mwishoni mwa juma lililopita jijini Kinshasa
na kundi la watu waliovalia sare za kawaida na wengine za jeshi
kwa
mujibu wa shirika hilo la VSV tukio hilo limetekelwa na kundi la watu
waliokuwa wamevalia sare mchanganyiko jeshi, polisi na za raia na
walikuwa katika gari la polisi na kupelekwa katika eneo
lisilojulikana bado.
Taarifa
zaidi zinasema kuwa watu hao 11 walikuwa kanisani wakifanya maombi
kwa ajili ya wagonjwa, na haijulikani lengo la tukio hilo, hata hivyo
shirika hilo limesema mmoja kati ya watekaji nyara alisema kuwa
wamepata kile walichokuwa wanatafuta.
Shirika
hilo linaombwa kuachiwa huru kwa watu hao.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire