Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuk Hagel na rais Barack Obama |
Waziri
wa ulinzi wa Marekani Chuk Hagel amefahamisha kwamba washauri wengine
130 wa kijeshi watatumwa nchini Iraq katika mji wa Erbil mji mkuu wa
Kurdistan kutathimini zaidi mahitaji ya watu wa kabila la wa Yazid
waliofukuzwa hivi karibuni katika makaazi yao na wapiganaji wa
kiislam wanataka kuunda taifa la Kiislam.
Kulingana
na taarifa ya jeshi la Marekani, washauri hao wa kijeshi watakuwa na
jukumu la kupanga na kuratibu miradi ya kibinadamu kwa wananchi hao
wachacha wa kabila la Yazid.
Wanajeshi
hao wanakamilishai idadi ya washauri mia tatu wa kijeshi ambao rais
Barack Obama alitangaza mwezi Juni kuwatuma nchini Iraq kusaidia
serikali ya Iraq kuzuia mashambulizi ya kundiu la Isil lililokuwa
likiendelea kuiteka miji kadhaa nchini humo.
katika
hatuwa nyingine vikosi vya Marekani tayari vimefanya operesheni 17
tangu siku ya Ijumaa kuzuia kundi la Isil kuendelea kusonga mbele
kwenye uwanja wa mapambano.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire