Serikali
ya Israel na kundi la Hamas la nchini Palestina wamekubaliana
kimsingi kutoa muda wa saa 72 kusitisha mapigano kwenye eneo la
ukanda wa Gaza baada ya kuongezeka kwa shinikizo toka jumuiya ya
kimataifa kuzitaka pande hizo kusitisha vita iliyodumu kwa siku 29
sasa.
Makubaliano
haya yamefikiwa mjini Cairo Misri, ikiwa ni siku tatu tu zimepita
toka makubaliano ya awali ya kutoa siku tatu za kusitisha vita
kushindikana kutokana na kila upande kuendelea na mapigano.
Marekani
imepongeza uamuzi huo na kusisitiza kuwa ni kundi la Hamas pekee
ndilo linalotakiwa kuheshimu makubaliano haya.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire