Viongozi
wa serikali ya Afrika Kusini wamesema watafanya uchunguzi kuhusu
uwepo wa taarifa za ubaguzi wa rangi katika shule za binafsi nchini
humo, baada ya wazazi kuwakilisha mashtaka kuhusu shule moja inayo
watenga wanafunzi kufuatia utaofauti wao wa rangi.
Ikiwa
ni siku chache baada ya mwaka wa shule kuanza nchini humo zaidi ya
familia 30 zimefungua kesi kupinga hatuwa hiyo kwenye shule moja
mjini Pretoria la Curro Foundation School ambapo watoto wa wazungu
walitenganishwa na watoto weusi.
Uongozi
wa shule hilo umeomba radhi hadharani na kubaini kwamba haujafanya
hivyo kwa nia ya ubaguzi wa rangi, bali ni kuwatenganisha kutokana na
mazingira ya utamaduni wao ili kila upande upate elimu kupitia lugha
yao.
Waziri
wa eilimu nchini humo Panyaza Lesufi ambae alizuru katika shule hilo
amesema hawezi kamwe kuvumulia kuona watoto wanarejshwa katika hali
waliokuwemo hadi mwaka 1994.
kamati
ya haki za binadamu nchini humo imesema imeanzisha uchunguzi kuhusu
shule hiyo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire