Serikali
ya Ujerumani imesisitiza kuendelea kushirikiana na nchi ya Tanzania
katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na
kuimarisha sekta ya usalama baina ya nchi hizi mbili.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake, rais wa Ujerumani, Joachim
Gauck amesema kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania
katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo kama ambavyo zimeendelea
kushirikiana kwa miongo kadhaa hivi sasa.
Kwa
upande wake rais wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete, amesema kuwa
Tanzania inajivunia kuwa na rafiki mzuri kama nchi ya Ujerumani na
kwamba nchi yake itaendelea kushirikiana na taifa hilo.
Akizungumzia
kuhusu usalama wa kikanda hasa tishio la ugaidi wa kundi la Al-Shabab
la nchini Somalia pamoja na makundi Mengine, rais Kikwete amesema
nchi yake imeendelea kubadilishana taarifa za kiintelijensia na
maofisa usalama wa Ujerumani na kwamba wataendelea kufanya hivyo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire