Bunge
la Niger limeidhinisha kwa kauli moja muswada wa sheria unaoruhusu
kutumwa kwa manjeshi nchini Nigeria kwa ajili ya kupambana na kundi
la wapiganji wa Boko Haram katika muktada wa uundwaji wa jeshi la
kikanda juu ya kurejesha usalama katika eneo nzima la mto Tchad.
Kulingana
na kauli ya mbunge wa upinzani Abdourahamane Chégou muswada huu
umeidhinishwa na wabunge waote 102 waliokuwepo bungeni, kauli ambayo
imethibitishwa pia na Mohamed Ben Omar, naibu spika wa bunge la
Nigeria ambae ameongeza kuwa wanajeshi 750 watatumwa huko kwa ajili
ya opersheni hiyo.
Wakati
wa upigaji kura wa muswada huu, spika wa bunge Amadou Salifou
amesema hatuwa hii inachukuliwa wakati mji wa Diffa kusini mwa Niger
mpakani na Nigeria makombora yanayorushwa na kundi la boko Haram
yaendelea kuanguka katika eneo hilo.
Niger
inawatuma wanajeshi wake nchini Nigeria wakati huu mvutano wa kisiasa
ukiendelea kutokota kutokana na hatuwa ya kuahirishwa uchaguzi kwa
sababu za kiusalama, jambo ambalo upinzani umepinga. Mwenda Mbijiwe
ni mchambuzi wa maswala ya Usalama anazungumzia kuhusu mashambulizi
ya kundi hili la Boko Haram.
Kundi
la Boko Haram kupitia kiongozi wake Abubakar Shekau amesema Nigeria
Haina uwezo wa kulishinda kundi hilo, na kutishia kufanya
mashambulizi zaidi katika nchi zinazotuma majeshi yake nchini Nigeria
kwa ajili ya kukabiliana na wapiganaji wa kundi hilo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire