Rais
wa Burundi Pierre
Nkurunziza amewafuta
kazi
Mkuu wa kitengo cha Ujasusi Meja
jenerali
Godefroid Niyombare, pamoja
Mkuu wa itifaki kwenye idara hiyo ya ujasusi Jenerali
Léonard Ngandakumana, pamoja
na mkuu wa usalama wa ndani Jenerali Sylvestre
Ndayizeye hatuwa
inayokuja ikiwa ni miezi mitatu tu baada ya kuteiliwa kwenye uadhifa
huo.
Msemaji
wa rais wa Burundi Leonidas Hatungimana hajaeleza sababu za kufutwa
kazi kwa kiongozi huyo ikiwa ni miezi mitatu kabla ya kuelekea kwenye
uchaguzi mkuu wa rais.
Hata
hivyo duru za kuaminika licha ya kukanushwa, zaelezwa kwamba hivi
karibuni maafisa hao walimshauri Rais Nkurunziza kutowania muhula wa
3, kwani ni hatuwa ambayo inaweza kuitumbukiza taifa hilo katika
janga la machafuko,
Inaelezwa
kuwa Nkurunziza alishauriwa na maafisa wake kuwa ikiwa atatangaza
kuwania, hatapata uungwaji mkono kutoka kwa wananchi na chama chake
cha CNDD FDD.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire