Muungano
wa jeshi la Iraq na Kikurdi linaungana kuchukua tena mji wa Mosul
uliodhibitiwa na kundi la Kiislamu la Islamic State.
Ripoti
kutoka Marekani zinasema wanajeshi 25,000 wanaandaliwa kukabiliana
na Islamic State ili kuukoboa mji wa Mosul.
Pentagon
inasema operesheni hiyo huenda ukafanyika mwezi Aprili na May katika
mji huo wa Kaskazini mwa Afrika ambao una kati ya wapiganaji elfu
moja na elfu mbili wa Islamic State.
Mji
Mosul ambao ulikuwa na wakaazi zaidi ya Milioni 2 kabla ya kutekwa na
Islamic State, umebaki na watu wachache.
Wakati
uo huo, wakuu wa majeshi kutoka zaidi ya Mataifa 20 wanakutana nchini
Saudi Arabia kujadili namna ya kuliimarisha jeshi la Iraq kupambana
na Islamic State.
Marekani
juma hili ilikuwa na Mkutano wa Kimataifa kuhusu namna ya kupambana
na makundi ya kigaidi na rais Barrack Obama alisema, nchi yake
haikabiliani na Uislamu bali na magaidi.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire