Pages

lundi 16 février 2015

JESHI LA SERIKALI NA WAASI WATUHUMIWA KUTUMIA WATOTO WADOGO JESHINI


Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Sudan Kusini yanazituhumu mbande mbili zinazokinzana nchini humo kusajili watoto wadogo walio na umri wa chini ya miaka kuni na mitatu kushiriki kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe, ripoti ambayo serikali ya Juba imekanusha vikali.

Ripoti ya mashirika hayo, imedai kuwa Serikali inashiriki kikamilifu katika kusajili vijana wadogo kujiunga na jeshi lake kwa hiari ama kwa kuwalazimisha wakati waasi wao pia wanatumia watoto kama wanajeshi katima vita vilivyodumu kwa zaidi ya miezi 14 hivi sasa.

Waziri wa habari wa Sudan Kusini, Michael Makuei ametupilia mbali madai ya ripoti hii akisisitiza kuwa jeshi lake bado lina nguvu ya kutosha kupigana bila kutumia watoto.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...