Rais
wa Nigeria ambae pia ni mgombea kwenye kiti cha urais nchini humo
Good luck Jonathan, anataraji kufanya kikao na waandishi wa habari
hii leo kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wanahabari nchini humo.
Hayo
yanajiri wakati Mwenyekiti wa tume ya Uchakuzi nchini Nigeria Profesa
Athahiri Jega ameshinikizwa kuachia ngazi ikiwa ni siku chache tu
baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo ambao ulikuwa umepangwa
kufanyika Februari mwaka huu na sasa umesogezwa hadi tarehe 28 mwezi
March mwaka huu.
Uamuzi
huo unakuja kufuatia kauli ya viongozi wa Usalama nchini humo
kudaikuwa hawakuandaliwa kwa zoezi hilo.
Vyanzo
vya kuaminika vinasema kuwa prof jega ameamuriwa na rais Good luck
Jonathan ambae ni mongoni mwa wagombea kwenye uchaguzi huo mkuu
kutoka chama cha PDP kwenda Likizo kuanzia mwezi March.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire