Shirika
la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Right Watch
limesema kuwa nguvu za kijeshi pekee hazitatosha kumaliza uasi wa
kundi la waasi wa kihutu wa Rwanda wa FDLR ambalo wapiganaji wake
wameendelea kujificha msituni licha ya kutakiwa kujisalimisha.
Kwenye
taarifa yake, Human Right inasema kuwa, mbali na kutumika kwa nguvu
za kijeshi dhidi ya wapiganaji hao, hatua nyingine pia zinapaswa
kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwasaka viongozi wa kundi hilo,
kubaini maeneo walikojificha na kuwashawishi wapiganaji wake
kuendelea kujisalimisha.
Ida
Sawyer ni mmoja wa viongozi wa shirika la Human Right Watch kwa nchi
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, kauli za viongozi haipashwaji kusalia pekee kwenye mashambulizi, lazima mbinu nyingine zitumike.
Kauli
hii ya Human Right Watch inatolewa wakati huu ambapo mwishoni mwa
juma jeshi la Serikali ya DRC tayari limeanza operesheni maalumu ya
kuwasaka na kuwasambaratisha wapiganaji wa FDLR ambao walikataa
kujisalimisha.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire