Viongozi
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekuwa wakikutana jijini Nairobi
nchini Kenya, kujadili na kuthathmini maendeleo ya Jumuiya hiyo
ikiwemo harakati za uundwaji wa shirikisho la kisiasa na matumizi ya
sarafu moja.
Marais
wa Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda na Uagnda wanasema juhudi kubwa
zinaendelea kuwaunganisha wananchi wa Jumuiya hiyo.
Mwenyekiti
mpya wa Jumuiya hiyo rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amesema
maendeleo ya jumuiya hiyo yanaonesha mshikamano kati ya wananchi wa
nchi hizo na kuhudi za viongozi.
Hata
hivyo, Rais Kikwete amesisitiza kuwa Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania
mwezi Oktoba na Burundi mwezi Juni itakuwa ni kipimo cha Demokrasia
katika nchi hizo mbili za Jumuiya hiyo.
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta aliyemaliza muda wake kama Mwenyekiti wa
Jumuiya hiyo naye amesisitiza umuhimu wa viongiozi wa Jumuiya hiyo
kuungana kwa manufaa ya wananchi wa Jumuiya hiyo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire