Serikali
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetupilia mbali makataa
yaliotolewa na Umoja wa Mataifa ulioipa majuma mawili serikali hiyo
kuwafuta kazi maofisa wake wawili wa juu wa jeshi kwa tuhuma za
kushiriki vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu,
Ma
Jenerali hao Bruno
Mandevu na
Sikabwe
Fall, ndio
waliopewa jukumu la Operesheni dhidi ya wapiganaji wa kihutu
waliopiga kambi kule mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Katika
taarifa yake kwa waandishi wa habari, msemaji wa Serikali ya DRC na
pia waziri wa habari, Lambert Mende, amesema kuwa Serikali yake
hiwafuti watu kazi kwa shinikizo na hasa maofisa wa juu wa jeshi
kwakuwa maofisa waliotajwa kwenye ripoti hiyo hawajashtakiwa kwenye
mahakama ya kijeshi.
Juma
hili Umoja wa mataifa umetishia kusitisha operesheni zake za pamoja
na majeshi ya Serikali ya DRC katika vita dhidi ya makundi ya waasi
mashariki mwa nchi hiyo iwapo utawala wa Kinshasa hautawafuta kazi
majenerali hao wa jeshi.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire