Saa
chache baada ya kuachiwa huru na mamlaka nchini Misri, mwandishi wa
habari wa kituo cha kimataifa cha Aljazeera raia wa Australia, Peter
Greste ameapa kuendelea kuwapigania waandishi wenzake ambao bado
wanashikiliwa gerezani kwa tuhuma za uhaini.
Familia
yake inasema kuwa, Peter ameahidi kuhakikisha kuwa anaendelea
kusimama na wenzake waliosalia gerezani akisisitiza kuwa hawana hatia
kama yeye ambavyo amekuwa akieleza kwa vyombo vya usalama nchini
Misri.
Waandishi
wengine wa kituo hicho wanaoshikiliwa ni pamoja na Mohamed Fahmy
mwenye uraia pia wa Canada pamoja na Baher Mohamed raia wa Misri
ambao walikamatwa kwa pamoja mwaka 2013 wakituhumiwa kushirikiana na
chama cha Muslim Brotherhood.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire