Pages

mardi 24 février 2015

MZOZO WAIBUKA KATIKA CHAMA FNL, JAQUES BIGIRIMANA AMFUTA UADHIFA WAKE KATIBU MKUU WA CHAMA HICHO


Emmanuel Miburo
Kamati ya watu 27 wanaotaka matawi ya chama cha FNL kuungana na kuwa kimoja, yamewataka Agathon Rwasa kuwa mwenyekiti wa FNL huku Jacques Bigirimana akiwa makam wake ili kuunda nguvu moja kwa ajili ya Uchaguzi.

Emmanuel Miburo katibu mkuu wa tawi la FNL ya Jacques Bigirimana linalo tambulika na serikali, amesema kamati ya watu 27 ambao wengi wao walikuwa ni kutoka tawi la Jacques Bigirimana na wajumbe 18, huku wengine 9 wakiwa ni kutoka tawi la FNL ya Agathon Rwasa.

Emmanuel Miburo amesema kamati hiyo ilifanya tathmini na kuomba muungano,lakini kwa mshangao mkubwa mwenyekiti Jacques Bigirimana hakutaka hata kusikiliza yaliomo katika ripoti hiyo ya kamati ilioundwa kwa kiasi kikubwa na wajumbe wa tawi lake.
Jacques Bigirimana

Kulingana na ripoti ya kamati hiyo, inaagiza viongozi hao kuunda kamati ya mseto na kuandaa kongamano March Mosi mwaka huu wa 2015 ili kuidhinisha nyadhifa mbalimbali za viongozi wa chama.

Katika majadiliano ya wajumbe wa kamati hiyo, walikuwa wamependekeza Jacques Bigirimana kuendelea kuwa mwenyekiti wa FNL, na kumteuwa Agathon Rwasa kuwakilisha chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa rais, lakini mwisho wa siku wajumbe hao waliafikiana kumteuwa Rwasa kuwa kiongozi na kuandaa kongamano March 1.

Mbali na kupinga hatuwa hiyo, Jacques Bigirimana amesema hajamtuma yeyote kumuwakilisha, na kuchukuw ahatuwa ya kumfuta kwenye uongozi katibu wake Emmanuel Miburo aliechaguliwa kupitia kongamano la chama hicho.

Agathon Rwasa
Jambo ambalo Miburo anasema Jacques Bigirimana hana uwezo wa kunfuta uadhifa kwa sababu sio yeye aliemteuwa, bali kongamano pekee la chama ndilo lenye uwezo wa kunfuta uadhifa wake, na kubaini kwamba upande wa tawi la Jacques Bigirimana, viongozi na wafuasi wote wanaridhia uwepo wa kongamano kuu la chama hicho, ispokuwa pekee Jacques Bigirimana.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...