Kansela
wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa, Francois Hollande hii
leo wanatarajiwa kuwa na mazungumzo na rais wa Urusi Vladmir Putin
katika juhudi zao za kujaribu kusaka suluhu ya machafuko mashariki
mwa nchi ya Ukraine, machafuko ambao Urusi inatajwa kuchochea.
Ziara
ya viongozi hawa wawili mjini Moscow imekuja saa chache baada ya
kufanya ziara kama hiyo nchini Ukraine ambako walikutana na rais
Petro Poroshenko ambaye baada ya mazungumzo yao alidai yalikuwa yenye
tija na yenye kutoa muelekea wa suluhu ya nchi yake.
Kansela
Merkel amesisitiza imani yake ya kuwa mzozo wa mashariki mwa Ukraine
unaweza kutatuliwa kwa njia za kidiplomasia kuliko kutumia nguvu za
kijeshi kuumaliza.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire