Chama
tawala nchini Burundi kimesisitiza kuwa Rais Pierre Nkrunzinza
atawania muhula wa tatu wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi June
mwaka huu, iwapo jina lake litapitishwa na chama kuwania nafasi hiyo.
Msimamo
huu wa chama tawala cha CNDD-FDD unatolewa wakati huu ambapo muungano
wa mashirika ya kiraia nchini Burundi yakitoa wito kwa rais
Nkurunzina kutowania muhula mwingine wa urais kuepusha kile
walichokiita machafuko nchini humo.
Msemaji
wa Rais, Willy Nyamitwe amesema kuwa rais Nkurunzinza atawania
kiti cha urais katika uchaguzi ujao iwapo kamati kuu ya chama
itamteua kufanya hivyo kulingana na katiba huku akiwaonya watu
wanaotaka kuchochea vurugu nchini humo.
Kiongozi huyo ameongeza kuwa vyombo vya usalama pamoja na vyombo vya sheria vitawachukulia hatua wale wote ambao watabainika kupanga njama za kuchochea machafuko nchini humo kabla na hata wakati wa uchaguzi mkuu.
Kiongozi huyo ameongeza kuwa vyombo vya usalama pamoja na vyombo vya sheria vitawachukulia hatua wale wote ambao watabainika kupanga njama za kuchochea machafuko nchini humo kabla na hata wakati wa uchaguzi mkuu.
Mashirika
ya kutetea haki za binadamu pamoja na mashirika ya kiraia zaidi ya
300 juma lililopita walianzisha kampeni maalumu ya kupinga hatua
yoyote ile ya kumuwezesha rais Nkurunzinza kuwania urais kwa muhula
wa tatu, jamabo ambalo wanasema iwapo litafanyika litakwenda kinyume
na katiba ya nchi.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire