Saa
chache baada ya kuanza kwa operesheni ya pamoja kati ya vikosi vya
nchi ya Chad, Cameroon na Nigeria dhidi ya kundi la Boko Haram,
majeshi hayol yamedai kuwauwa zaidi ya wapiganaji 200 wa kundi hilo.
Kwa
mujibu wa taarofa iliyotolewa na jeshi la Chadi, imesema kuwa
wanajeshi wake 9 walipotesha maisha huku wengine zaidi ya 21
wamejeruhiwa kwenye mapigano ya ardhini yaliyodumu kwa saa kadhaa
kwenye mji wa Gambori.
Mapigano
haya yametokea baada ya serikali ya Chadi kutuma zaidi ya wanajeshi
elfu 2 kwenye eneo la mpaka wa nchi hiyo na Nigeria ambako wapiganaji
wa kundi la kiislamu la Boko Haram walikuwa wamekita kambi.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire