Ujumbe
wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO
unapongeza dhamira ya serikali ya DRC kuchukua pekee jukumu la
kuwasaka waasi wa kihutu wa rwanda wa FDLR walioko Mashariki mwa nchi
hiyo kama alivyoamua rais Joseph Kabila.
Kaimu msemaji wa Ujumbe huo Umoja Charles Bambara amesema kuwa pamoja na kupongeza hatua hiyo, MONUSCO itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kutimiza agizo waliokabidhiwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Kulingana
na Msemaji huyo, MONUSCO itaendelea kusaidia jeshi la Congo FARDC
katika shughuli nyingine za kijeshi dhidi ya vikundi vingine vyenye
kumiliki silaha mashariki mwa DRC ikiwa ni pamoja na Kivu ya
Kusini, Kivu kaskazini , Butembo, Katanga na mahali pengine.
Kauli hiyo haitofautiani na ile ya Msemaji wa Serikali ya Congo Waziri Lambert Mende ambaye hapo jana katika mkutano na waandishi wa habari amebainisha kuwa MONUSCO kutimiza wajibu wake bila ya kutegemea Jeshi la DRC dhidi ya makundi yote yenye kumiliki silaha kwa vile ni sehemu ya majukumu ya Ujumbe huo.
Kwa
upande wake, MONUSCO pia imeahidi kuendelea kutimiza wajibu wake
kama ilivyo azma ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika
shughuli nyingine za kijeshi kwa kushirikaiana na jeshi la DRC
amesema Charles Bambara.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire