Marekani
imewasilisha kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mapendekezo
ya vikwazo kwa viongozi wanaohusika na mzozo nchini Sudani Kusini
inayokabiliwa kwa sasa na mzozo wa kivita na mauaji ya kikabila
yanayoendelea kushuhudiwa.
Muswada
huo unaagiza vikwazo kwa viongozi walengwa wa moja kwa moja, kuziuia
mali zao, na kuwanyima haki ya kusafiri wale wote wanaotishia amani
na utulivu, na wanaozuia misaada kuwafikia walengwa nchini humo.
Mbali
na vikwazo hivyo kwa viongozi husika na mzozo nchini Sudani Kusini,
Marekani inapanga pia kulishinikiza baraza la usalama la Umoja wa
mataifa kuiwekea vikwazo vya silaha nchi hiyo. Umoja wa Ulaya unaunga
mkono mapendekezo haya.
Hata
hivyo viongozi wa mrekani wamegawanyika kutokana na pendekezo hilo,
upande mmoja unaunga mkono pendekezo hilo, huku mwingine ukiona kwamba vikwazo vya silaha vitamdhoofisha zaidi
rais Salva Kiir dhidi ya mpinzani wake Riek Mashar.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire