Jeshi
la ulinzi nchini Kenya hii leo limetangaza kufanikiwa kuwaokoa raia
wake wawili waliokuwa wanashikiliwa mateka toka mwaka 2011 na
wanamgambo wa kundi la Al-Shabab nchini Somalia.
Msemaji
wa jeshi la ulinzi nchini humo, Kanali Willy Wesonga amethibitisha
jeshi la nchi yake kuwaokoa raia hao wawili waliotambuliwa kwa majina
ya James Kairie Gichuhi aliyekuwa dereva wa shirika la Care
International na Daniel Njuguna Wanyoike anayeelezwa kuwa mfanyakazi
wa shirika moja la usafirishaji dawa nchini humo.
Raia
hao waliokolewa na wanajeshi wa Kenya walioko nchini Somalia chini ya
mwavuli wa vikosi vya Umoja wa Afrika AMISOM ambapo walikuwa
wanashikiliwa mateka na wanamgambo hao kaskazini mwa nchi ya kenya
kwenye mpaka na nchi ya Somalia toka mwaka 2011.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire