Kundi
moja la kidini nchini Ethiopia limetangaza kuwa mwezi huu litafanya
maandamano makubwa nchini humo kupinga vitendo vya ushoga na usagaji
ambavyo wamesema vinaendelea kukua kwenye nchi za pembe ya Afrika.
Maandamano
haya yameitishwa ikiwa imepita miezi kadhaa toka nchi za Uganda na
Nigeria zipitishe sheria kali zinazokataza ndoa za watu wa jinsia
moja wala vitendo vinavyohusiana na usagaji.
Mkuu
wa muungano wa makanisa ya kikristo nchini humo, Dereje Negash
amesema umoja wao utaitisha maandamano hayo mwezi huu kuunga mkono
juhudi za Serikali kupinga vitendo hivyo nchini Ethiopia na kwenye
nchi za pembe ya Afrika.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire