Balozi wa Marekani UN Smantha Power |
Balozi
wa Marekani Kwenye Umoja wa Mataifa Samantha Power amefanya ziara
fupi nchini Burundi hapo jana na amekutana kwa mazungumzo na rais wa
taifa hilo Pierre Nkurunziza ambapo alikuwa amemletea risala ya rais
wa Marekani Barack Obama.
Power
ambaye amepongeza Burundi kwa hatuwa yake ya kushiriki katika kikosi
cha kulinda amani nchini Somalia, na hivi karibuni nchini Jamhuri ya
Afrika ya Kati, amemueleza rais Nkurunziza kuhusu Marekani kuwa na
wasiwasi kuhusu vitendo vya uvunjifu wa haki ya kujieleza kwa
wananchi na wanasiasa ambavyo vinawakumba wanasiasa wa Upinzani,
vyombo vya habari na mashirika ya kiraia.
Samantaha Power amemtaka rais Nkurunziza ambaye anataka kuwania muhula wa tatu licha ya katiba ya nchi hiyo kutomkubalia, kusitisha nia yake hiyo na kuheshimu katiba.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire